Vibwanga vya maisha
Hivi
karibuni tumeweza kuona wanasiasa wetu wakiziendesha kampeni zao katika sehemu
tofauti za nchi.Vinara wa CORD Raila Odinga na Kalonzo Musyoka wamekuwa
wakiendeleza kampeni zao katika sehemu za pwani na magharibi mwa nchi.
Uhuru na
Ruto Ambao ni vinara wa mlengo wa Jubilee pia wao hawajaachwa nyuma kwani
wamekuwa wakiziendeleza kampeni zao sehemu za kati na bonde la ufa hivi
karibuni.
Jubilee kwa
hivi sasa wanaonekana kuwa na mwelekeo kwani kufikia sasa hivi wamechagua
atakaye peperusha bendera yao kupitia chama ambacho kilizindiliwa hivi karibuni
cha Jubillee Alliance Party(JAP).
Mlengo wa
Cord kwa hivi sasa unaonekana kutingisika kwani
viongozi wa mlengo huu wamekihama chama na kujiunga na chama kipya cha
JAP
Tumemuona
kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka akitoa matamshi ambayo ukiyazingatia sana
utafahamu kuwa anataka kujiondoa kwenye mlengo wa Cord.Kalonzo alisema kuwa
amempa Kinara wa ODM Raila Odinga mara nyingi kuwania kiti cha Urais bila
mafanikio.
Haya maneno
ukiyatafakari kwa undani yana maana kuwa Kalonzo amechoka na mlengo wa CORD na
anataka kupewa nafasi kugombea kiti cha
Rais ila tu asiwekwe kama mahindi kwenye ukumbi.
Mlengo wa
jubilee unaonekana kuwa na mwelekeo kwani wanakula nyama huku wengine wakimeza
mate.Mlengo wa CORD unafaa uwe na uhusiano mzuri kati ya wanavyama wote ili
wawe na safari njema katika kuendeleza kampeni zao.