Tuesday, 4 October 2016

VIBWANGA VYA MAISHA



Vibwanga vya maisha
Hivi karibuni tumeweza kuona wanasiasa wetu wakiziendesha kampeni zao katika sehemu tofauti za nchi.Vinara wa CORD Raila Odinga na Kalonzo Musyoka wamekuwa wakiendeleza kampeni zao katika sehemu za pwani na magharibi mwa nchi.
Uhuru na Ruto Ambao ni vinara wa mlengo wa Jubilee pia wao hawajaachwa nyuma kwani wamekuwa wakiziendeleza kampeni zao sehemu za kati na bonde la ufa hivi karibuni.
Jubilee kwa hivi sasa wanaonekana kuwa na mwelekeo kwani kufikia sasa hivi wamechagua atakaye peperusha bendera yao kupitia chama ambacho kilizindiliwa hivi karibuni cha  Jubillee Alliance Party(JAP).
Mlengo wa Cord kwa hivi sasa unaonekana kutingisika kwani  viongozi wa mlengo huu wamekihama chama na kujiunga na chama kipya cha JAP
Tumemuona kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka akitoa matamshi ambayo ukiyazingatia sana utafahamu kuwa anataka kujiondoa kwenye mlengo wa Cord.Kalonzo alisema kuwa amempa Kinara wa ODM Raila Odinga mara nyingi kuwania kiti cha Urais bila mafanikio.
Haya maneno ukiyatafakari kwa undani yana maana kuwa Kalonzo amechoka na mlengo wa CORD na anataka  kupewa nafasi kugombea kiti cha Rais ila tu asiwekwe kama mahindi kwenye ukumbi.
Mlengo wa jubilee unaonekana kuwa na mwelekeo kwani wanakula nyama huku wengine wakimeza mate.Mlengo wa CORD unafaa uwe na uhusiano mzuri kati ya wanavyama wote ili wawe na safari njema katika kuendeleza kampeni zao.